Jan 18, 2014

Wazayuni watiwa kiwewe na makombora ya Hizbullah

Muasisi wa mpango wa makombora katika Wizara ya Vita ya utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri  kwamba Hizbullah  ya Lebanon ina makombora yenye nguvu na wapiganaji wa kundi hilo wana nguvu za kutosha.  

Uzi Rabi ameongeza kuwa, utawala wa Israel hivi sasa umeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na  taathira za nguvu za makombora ya Hizbullah dhidi ya Israel na kusisitiza kuwa, kuna uwezekano mkubwa  kwa makombora hayo kuwa tishio la kiistratijia kwa utawala huo. 

Uzi Rabi amedai kuwa Hizbullah hivi sasa inapanga mikakati ya kumiliki makombora ya masafa marefu. 

Hivi karibuni Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD lilitoa taarifa ya mwaka na kueleza kwamba Hizbullah inazidi kupata uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Lebanon na kusisitiza kuwa harakati hiyo ya muqawama licha ya kukabiliwa na mashinikizo mbalimbali, hivi sasa iko katika nafasi nzuri na nguvu za harakati  hiyo  zimeonekana nchini Syria. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, wapiganaji wa Hizbullah walielekea nchini Syria na kupigana bega kwa bega na majeshi ya serikali  dhidi ya makundi ya kigaidi na yale yanayowakufurisha Waislamu wengine nchini humo.

0 comments:

Post a Comment