Jan 17, 2014

TUWAHURUMIE WATOTO-KHUTBA YA IJUMAA


Waislamu wamekumbushwa kwamba kuwahurumia watoto ni moja katika kufuata mafundisho ya Mtume S.A.W.

Akitaffsiri khutba ya Ijumaa iliyosomwa hivi punde katika Msikiti wa Qiblatain,Sheikh Abdallah Haruon (Imamu) alisema tukiwa tupo katika miezi ya kumuadhimisha Mtume S.A.W,tusisahau kuwahurumia watoto.

Aliendelea kusema kwamba katika maisha yake Mtume S.A.W alikuwa karibu sana na watoto,lakini mbali ya kuwapenda pia aliwahurumia.


"Ndugu zangu Waislamu,Mtume wetu alikuwa na tabia ya kurefusha Swala.lakini mara kadhaa alipokuwa anaswali kisha akiwa ndani ya swala anamsikia mtoto analia,basi mtume anafupisha Swala kwa ajili ya kumliwaza na kumfariji mtoto"alisema.

Sheikh Abadallah hakusita kumtaja Swahaba wa Mtume Anas bin Malik kwamba ametamka bayana akisema,"Naapa kwa jina la ALLAH,sijawahi kumuona mtu mwenye huruma kwa watoto,zaidi ya Mtume S.A.W"

Alikhitimisha kwa kuwataka wazazi kuwa na huruma za kweli kwa watoto ili kuyaenzi kivitendo mafundisho ya Mtume S.A.W.

0 comments:

Post a Comment