Oct 1, 2014

Mtandao wa kijamii wazua vita vya kidini nchini India

ind
Vita vimezuka kati ya waislamu na wahindi katika mji wa Gujarat huko India baada ya picha kuwekwa katika mtandao wa kijamii unaokosea dini ya Kiislamu kughadhabisha wakaazi wa eneo hilo.
Wakaazi wa dini hizo mbili wamerushiana mawe na kuchoma magari na kusasabisha wengi kujeruhiwa huku mmoja akidungwa kisu katika vurugu hilo.

Afisa mkuu katika eneo hilo amesema kuwa huduma za mtandao zote zikiwemo za simu zimesimamishwa hadi kesho ili kupunguza uenezi wa hasira kwa wananchi.


Kamishna wa polisi katika eneo hilo D.J Patel amesema mwanamume aliyeweka picha hiyo kwa mtandao wa kijamii ametiwa mbaroni pamoja na watu 200 wanaoshukiwa kuanzisha vita hivyo

0 comments:

Post a Comment