Oct 3, 2014

MAHUJAJI KUSIMAMA ARAFA LEO

 Image result for arafat makkah
 Vilima Vya Arafa.

Mamilioni ya Mahujaji waliofurika katika mji wa Makka hivi sasa wana miminika katika viwanja vya Arafa vilivyopo pembezoni mwa mji wa Makkah.

Kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu leo ni mwezi tisa Dhul Hijjah kwa mujibu wa mwandamo wa mji wa makkah.

Mahujaji hao mbali ya kutoka maeneo mbalimbali duniani wengi wao wakitokea katika (kituo) mji wa Minaa ambapo waliwasili hapo tokea jana.

Kisimamo cha Arafa kitaanza mara baada ya kupinduka jua ambapo baada ya Al asri misururu ya Mahujaji itaondoka kuelekea Muzdalifa ambapo watalala hapo.

Kesho Alfajiri Mahujaji wataondoka Muzdalifa na kurejea Minaa kwa ajili ya kuendelea na Jbada ya Jamaraat.

Ibada ya Hijjah ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu

Munirablog inawatakia mahujaji wote afya njema na hijja mabruul.



Image result for arafat makkah


Image result for arafat makkah
Minaa

0 comments:

Post a Comment