Oct 3, 2014

Watu kadhaa wauawa katika mapigano CAR

Watu wasiopungua sita wameuawa katika shambulizi lililofanywa katika kambi ya wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Kwa mujibu wa habari, shambulizi hilo limetokea jana katika mji wa Bambari baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi moja ya wakimbizi mjini hapo na kusababisha watu wengine pia kujeruhiwa. Bado haijafahamika waliotekeleza shambulizi hilo.
Mwanzoni mwa wiki hii zaidi ya watu 11 waliuawa katika mapigano makali kati ya wapiganaji wa Kikristo wa Anti-Balaka na wale wa muungano wa Seleka katika mji wa Ngakobo uliopo kilomita 60 kutoka mji huo wa Bambari. 

Kwa mujibu wa mashuhuda wote waliouawa kwenye mashambulizi hayo ni wanachama wa Seleka. 

Licha ya kuteuliwa Mahamat Kamoun, ambaye ni Mwislamu kushika wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, bado machafuko yangali yanaendelea kushuhudiwa siku hadi siku katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. 

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye lindi la mapigano mwishoni mwa mwaka 2012 huku waathirika wakubwa wa mapigano hayo wakiwa ni Waislamu.

0 comments:

Post a Comment