Jul 21, 2013

TUSIWAHUSUDU WATOTO WALIOHIFADHI QUR AAN.-DR SULEYMAN

Sheikh.Ally Bassaleh akiwahutubia waislamu katika mashindano hayo.
  • TUWANYENYEKEENI NA TUWAUNGE MKONO.
  • MASHINDANO YA QUR AAN YAFANA.
  • ZAWADI ZA MAMILIONI YA PESA ZATOLEWA.

Na mwandishi wetu wa munira.
Waislamu wanetakiwa kuwa na silka ya kuwaheshimu,kuwapenda na kuwaunga mkono watoto waliohifadhi Qur aan na kuacha tabia ya baadhi ya waislamu kuwahusudu watoto hao kwa kuwaonea wivu.

Hayo yamesemwa na Dokta Suleyman Ally Yusuph ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano ya kuhifadhi qur aan yaliyomalizika hivi punde katika ukumbi wa diamond jubilee uliopo upanga jijini dare s salaam.

Akiongea katika hafla hiyo Dokta Suleyman ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuhifadhi Qur aan Tnzania amesema,Mtume S.A.W amekataza tabia ya kuwasimamia watu,lakini kwa kuwa hawa watoto wamehifadhi Qur an yote tena miongoni mwao ni walemavu wa macho,hawa inafaa kuwanyenyekea,naomba nieleweke,sipingani na maneno ya Mtume S.A.W laa hashaa ,alisema.

“Leo badala ya kuwapenda watoto kama hawa,au kufanya jitihada ili mtoto wako awe kama watoto hawa badala yake miongoni mwetu tunawahusudu kwa njia mbalimbali”mwisho wa kumnukuu.

Akiongea katika hafla hiyo,Sheikh Ally Bassaleh alisema,”katika ulimwengu huu,Qur aan ndiyo kitabu pekee chenye miujiza na hakuna kitabu chochote kinachoweza kuhifadhiwa chote hata na watu wenye macho yao sembuse walemavu wa macho,tumeshuhudia hivi punde watoto walemavu wa macho wakiwa wamehifadhi qur aan kwa njia tofauti”.

Aliwanasihi Waislamu wasiishie katika kuhifadhi pekee bali pia wazingatie yaliyomo katika qur aan.

Katika mashindano hayo zawadi za pesa na vitu mbalimbali ikiwemo Vyarahani,Pikipiki,Bajaji,Baiskeli zilitolewa kwa washindi,ambapo Abdul hamiid Masuod alifanikiwa kuwa mshindi wa kwanza kwa wanaume waliohifadhi  Juzuu 30 ambapo alipata pesa taslimu Shilingi Laki tatu na Bajaji,sambamba na suraiyyah ally baker mshindi wa kwanza kwa wanawake ambaye pia alipata bajaji na pesa taslimu shilingi laki tatu.
Namshukuru mungu ameniwezesha kufikia malengo yangu,hii pesa nitaitumia katika kujiendeleza na elimu ya kimazingira (shule) na hii Bajaji nitaifanya kuwa ni kitega uchumi”,aliongea Abdul hamiid Masuod mbaye ni Mwanafunzi katika Madrasat Baytul Maqdis ya Ubungo

Taasisi ya Aisha Sururu Foundation chini ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Aisha Sururu ndiyo Taasisi iliyoandaa mashindano hayo,na huu ni mwaka wa saba mfululizo toka waanzishe mashindano hayo.
 MABRUOK A'LAYK"NDIVYO ANAVYONEKANA KUSEMA MGENI RASMI WAKATI AKIMKUMBATIA MSHINDI WA KWANZA WA JUZUU 30 KWA UPANDE WA WANAUME KIJANA ABDUL HAMIID MASOUD KUTOKA UBUNGO JIJIN DAR ES SALAAM.

 MHE MGENI RASMI AKIMKABIDHI ABDUL HAMIID MASUOD (MSHINDI WA KWANZA WA JUZUU 30) KITITA CHA PESA NA BAJAJI.
 "KWA KWELI SIWEZI KUZUNGUMZA,KWANI NIMECHOKA SANA NA NINA FURAHA KUPITA KIASI,ILA NAMSHUKURU MUNGU MAMBO YAMEENDA VIZURI,NDIVYO ALIVYOSEMA BI AISHA SURURU ALIPOTAKIWA KUFANYA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA MUNIRABLOG LEO HII.
PICHA JUU NI BINTI ALIYEHIFADHI JUZUU KUMI KATIKA MTINDO WA TAHQIIQ  HALI YA KUWA NI MLEMAVU WA MACHO NA MIGUU NA MIKONO,ALLAHU AKBAR

PICHA CHINI NI MSHINDI WA TATU WA JUZUU KUMI BI ASIA MUHUNZI FAQIH (UMRI MIAKA 8) AKIWA AMESHIKILIA KITITA CHA SHILINGI LAKI SITA ZIKIWA NI ZAWADI ZA USHINDI WAKE,AMEMUELEZA MWANDISHI WA MUNIRABLOG KWAMBA HAJUWI ATAZIFANYIA NINI PESA HIZO ILA HATOMPA BABA WALA MAMA BALI ATAMPA USTAADH WAKE WA MADRSAT JAWHARIYYAH YA VINGUNGUTI,DAR ES SALAAM