Jan 15, 2014

Kura ya maoni ya Misri yaingia siku ya pili

Wananchi wa Misri leo wanajitayarisha kushiriki katika siku ya pili na ya mwisho ya kura ya maoni ya katiba mpya, huku watu zaidi ya 10 wakiripotiwa kuuawa hapo jana katika machafuko.

Maelfu ya askari polisi na wanajeshi wamepelekwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuzuia machafuko karibu na vituo vya kupigia kura. 

Hapo jana katika siku ya kwanza ya kura ya maoni kulishuhudiwa ghasia zilizotokana na kukandamizwa waandamanji wanaopinga jeshi ambapo watu 11 waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa.

 Zaidi ya watu milioni 52 wanatarajiwa kushiriki katika kura hiyo ya maoni inayofanyika kwa muda wa siku mbili nchini Misri. 

Rasimu ya katiba hiyo imeandaliwa na serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi lililompindua rais halali aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Mursi.

0 comments:

Post a Comment