Jan 15, 2014

Askari wa Israel wabomoa nyumba za Wapalestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamebomoa nyumba za raia wa Palestina katika bonde la Jordan na kuwaacha wanavijiji bila ya makazi katika majira haya ya baridi kali. 

Maafisa wa utawala wa Kizayuni pia wametwaa makazi ya muda na misaada yote ya kibindamu waliyokuwa wamepewa raia wa Kipalestina ambao nyumba zao zimebomolewa na jeshi la Israel.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema yanatiwa wasiwasi na kuongezeka ubomoaji wa nyumba za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni. 

 Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na masuala ya kibinadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (OCHA) ilitoa misaada hiyo ya kibinadamu kabla ya maafisa wa Israel kukisambaratisha kijiji kizima katika eneo la Jiftlik katika bonde la Jordan. 

Jeshi la utawala wa Kizayuni limelitangaza eneo hilo kuwa ukanda wa kijeshi uliofungwa huku vyombo vya habari na makundi ya kutetea haki za binadamu yakikatazwa kuingia katika eneo hilo.

0 comments:

Post a Comment