Jan 15, 2014

Mabinti waozwa chini ya umri wa kisheria huko Uturuki

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa nchini Uturuki unaonyesha kuwa theluthi moja ya mabinti huko mashariki na kusini mashariki mwa nchi hiyo wanaolewa chini ya umri wa kisheria. 

Utafiti huo uliofanywa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya KAMER unaonyesha kuwa sehemu kubwa ya mabinti hao wana umri wa chini ya miaka 15 ambapo ndoa nyingi hufanyika khususan katika maeneo ya vijijini huko mashariki na kusini mashariki mwa Uturuki, jambo linalotia wasiwasi sana.
Ripoti ya Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya KAMER imewataka viongozi wa Uturuki kuchukua hatua za haraka ili kuzuia ndoa za watoto katika maeneo hayo. 

Utafiti huo mpya ulifanywa kufuatia mazungumzo yaliyofanyika kati ya taasisi hiyo na wanawake elfu sitini katika mikoa 23 ya mashariki na kusini mashariki mwa Uturuki. 

Umri wa kufunga ndoa nchini Uturuki hivi karibuni uliongezwa kutoka miaka 15 hadi 17. Hii ni katika hali ambayo baadhi ya weledi wa mambo wanaamini kuwa kuongezwa umri wa kufunga ndoa tu huko Uturuki hakutoshi kwa ajili ya kukabiliana na suala hilo la ndoa za mapema.

0 comments:

Post a Comment