Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jana alilituhumu jeshi na waasi wa Sudan Kusini wanaoongozwa na Riek Machar, Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo kuwa wanaiba misaada ya chakula na magari yanayotumika kusambazia chakula huku nchi hiyo ikikaribia kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Ofisi ya habari ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Ban Ki-moon anatiwa wasiwasi na kuongezeka idadi ya wahanga kutokana na kuendelea mapigano huko Sudan Kusini, kukiwemo ripoti waliyoipokea jana Januari 14 kuhusu vifo vya watu 300 waliozama katika ziwa Nile wakati wakikimbia mapigano katika mji wa Malakal.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali hatua ya vikosi vya jeshi la Sudan Kusini na waasi wa nchi hiyo ya kuiba magari, misaada ya chakula, na suhula nyingine za kibinadamu.
0 comments:
Post a Comment