Nov 1, 2013

WAISLAMU Tuwe na Nidhamu

SHEIKH OMAR AL HAD WAKATI AKIHUTUBU KATIKA SWALA YA IJUMAA,HIVI PUNDE.


Waislamu nchini wametakiwa kuwa na nidhamu kwa kuwa ndiyo msingi bora katika dini.

Nasaha hizo zimetolewa hivi punde na Sheikh Omar Alhad ambaye ni imamu wa msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Dar es salaam.

Akiwahutubia mamia ya waumini katika khutba ya swala ya ijumaa,amesema waislamu tumepoteza sifa ya nidhamu aliyotuachia mtume s.a.w kitu ambacho kitatugharimu sana.

Maswahaba waliokaa na Mtume kwa kipindi kifupi waliweza kufaidika mno kutokana na wao kuwa na nidhamu ya kufuata mafunzo ya Mtume S.a.w

"leo sisi tuna hazina kubwa ya Elimu ya Qur aan na mafunzo ya Mtume s.a.w lakini kwetu yamekuwa hayana faida kwa kuwa hatuna nidhamu ya kuyafuata mafunzo hayo".

Akiongea kwa hamasa kubwa Sheikh Omar alimtolea mfano Swahaba Abdullahi Ibn Abbas ambaye alizaliwa miaka mitatu kabla ya Hijra na wakati Mtume saw anafariki,swahaba huyo alikuwa na miaka 13.

Aliendelea kusema licha ya Abdullahi Ibin Abbaas kuishi na mtume saw kwa muda mchache (miaka 13 tu) lakini hakuwa na tabia ya kuchagua cha kufuata kutoka kwa Mtume s.a.w.

Aliongeza kwa kusema nidhamu njema za Abdullahi Ibni Abbas zilimfanya awe amehifadhi hadithi 1660 ndani ya muda mfupi alioishi na mtume saw.

"leo wanazuoni mbalimbali duniani wana tegemea tafsiri yake (Tafsir ya Qur aan ya Ibni Abbas)"alisema.

Kwa masikitiko katika kuonesha upeo wa kutokuwa na nidhamu Sheikh Omar alisema,"imejengeka tabia kwa baadhi ya Waislamu kukodi mabaunsa kwa ajili ya kufanya vurugu katika misikiti,jambo hili ni khatari kwenu"

"Siwatukani lakini nawaambia wanaokodi mabaunsa ni wajinga,na hao mabaunsa wenyewe pia ni wajinga"mwisho wa kumnukuu.

Hakusita kuwakumbusha nguvu kubwa alizokuwa nazo mfalme wa Ethiopia Abraha ambaye alidhamiria kuivuruga nyumba ya ALLAH lakini wakatutana na nguvu kubwa ya Allah na kusambaratishwa.
 SEHEMU YA WAUMINI WAKISIKILIZA KHUTBA,KATIKA MSIKITI WA KICHANGANI.

 MWANANGU,KUONGOZA BINAADAMU NI KAZI NGUMU,MUHIMU UVUMILIVU NA KUMUOMBA ALLAH,NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA SHEIKH JUMA MBUKUZI


0 comments:

Post a Comment