Nov 2, 2013

Michango ya Msikiti Wa Kichangani Yafikia Milioni Tisa

SHEIKH OMAR AL HAD IMAM WA MSIKITI WA KICHANGANI,AKISOMA MAPATO YA MICHANGO.

Mpango maalumu wa kujiletea maendeleo bila ya kusubiri wafadhili unaoendeshwa katika msikiti wa kichangani, umefikia hatua mzuri baada ya zaidi ya Milioni Tisa kupatikana ndani ya siku sitini na moja (61).

Akitoa taarifa ya mapato ya michango hiyo jana baada ya Swala ya Ijumaa,Imamu wa Msikiti huo sheikh Omar Al had alisema hadi kufikia tarehe 31/10/2013 jumla ya shilingi Milioni Tisa Laki Nne Sitini na Sita na Mia sita Khamsini (9,466,650/-) zimepatikana.

Alisema "kwa wiki hii (wiki iliyoishia jana) makusanyo yameshuka,pamoja na hivyo tusikate tamaa ,kwani wajibu wa kuleta maendeleo yetu ni sisi wenyewe"

"Ilikuwa tuna wasubiri wenzetu waliokwenda Makkah katika ibada ya hijja,kwa kuwa wamerudi basi muda si mrefu mutafahamishwa hatua zitakazo fuata"alisema

Aidha aliwataka waumini waongeze kasi ya kuchangia na wawapuuze wale wote wanaobeza au kutaka kukwamisha jambo hili kwa maslahi yao binafsi.

Michango hiyo ilibuniwa na Sheikh Omar Al had kwa kutumia kauli mbiu ya wakati wa mabadiliko ni sasa,ambapo ilianza rasmi tarehe 02/09/2013.

Wakati huo huo Sheikh Omar Al had alikanusha madai ya kwamba michango hiyo inamnufaisha yeye na blog yake ya munira.

"Nimefurahi sana kuja kwa mkurugenzi wa munira blog,ndugu waumini huyu ndiye mkurugenzi wa munira blog,(wakati huo mkurugenzi huyo akichukua matukio kwa njia ya picha).Alisema.

Aliendelea kusema "Madrasa hii imejitolea kuanzisha blog kwa lengo la kuwapa habari waislamu,na wanafanya kazi katika mazingira magumu sana,naomba mufahamu blog hii si yangu wala si ya mama yangu kama wanavyosema wasiotutakia kheri".mwisho wa kumnukuu.

 SHEIKH YUSUF KUNDECHA AKITIA NENO KATIKA KUKAZIA MICHANGO HIYO.


0 comments:

Post a Comment