Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu
waliokufa kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwenye nchi za Afrika
Magharibi imefikia watu 467 na kuonya kuwa idadi hiyo huenda
ikaongezeka.
Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo uliozikumba nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone, WHO inasema kuwa mpaka sasa wamebaini kuwepo kwa maambukizi mapya zaidi ya watu 759 kwenye ukanda huo hali inayoogofya kuhusu kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo.
Idadi hii mpya inafanya kufikia kiwango cha asilimia 38 cha maambukizi mapya ukilinganisha na kiwango cha asilimia 27 mwezi Aprili mwaka huu wakati Shirika la Afya Duniani lilipotoa takwimu za mwisho kuonesha mwenendo wa ugonjwa huo ambao ulionekana kana kwamba umedhibitiwa.
Mtu aupatapo ugonjwa huu huweza kuwa na homa kali, maumivu ya viungo, kutapika na kuhara na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya ogani za mwili na kutokwa damu mfululizo.
0 comments:
Post a Comment