Akitangaza nafasi ya Katibu mkuu ambayo ilikua na mgombea mmoja tu Maalim Seif Sharif Hamad ambapo jumla ya 678 zilipigwa na hakuna kura ilioharibika.
Amesema kura ziliopigwa na kumkataa Maalim Seif kutokuwa katibu mkuu wa Chama hicho ni kura 3 na kura zilizomkubali ni 675 sawa na asilimia 99.57.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa CUF msimamizi wa uchaguzi amemtangaaza Mh.Juma Duni Haji kuwa mshindi wa nafasi hio kwa kupata kura 662 sawa na asilimia 99.25. kura zilizopigwa na kumkataa ni 5 sawa na asilimia 0.75.kwa upande wa kura zilizoharibika ni 0.
Aidha msimamizi huyo amemtangaaza Prf.Ibrahim Harouna Lipumba kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama hicho kwa kupata kura 659 sawa na asilimia 95.5,kura zilizomkataa ni 0 na mpinzani wake ambae ni Chifu Lutalosa Yemba ambae amepata kura 30 sawa na asilimia 4.5.
Wakati akitoa shukrani Katibu mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuwa na imani naye.
Amesema atahakikisha anaendeleza gurudumu mpaka chama hicho kitakapoingia madarakani mwaka 2015.
Mkutano huo mkuu unendelea tena leo kwa ajili ya kuwachagua wajumbe wa Baraza kuu Taifa CUF.
0 comments:
Post a Comment