Apr 23, 2014

BARAZA LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR (BATAKI) LIMELAANI KAULI ZA KICHOCHEZI DHIDI YA WAISLAMU BUNGE LA KATIBA.


BARAZA LA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR (BATAKI) LIMELAANI KAULI ZA KICHOCHEZI,CHUKI NA UADUI ZILIZOTOLEWA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA DHIDI YA WAISLAM WA ZANZIBAR.



KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA KWA VYOMBO VYA KHABARI NAKUSAINIWA NA AMIRI WA BARAZA HILO SAMAHATU SHEIKH ALI ABDALLAH SHAMTE MARA BAADA YA KUMALIZIKA KIKAO CHAKE KILICHOJADILI KAULI HIZO ZILIZODAIWA KUTOLEWA NA MAWAKALA WA KANISA NDANI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA IMEBAINIKA KUWA BAADHI YA WAJUMBE WANASIMAMIA AJENDA YA KANISA YAKUENDELEA KUIDHIBITI ZANZIBAR KWA KUTUMIA KIVULI CHA MUUNGANO BADALA YAKUJADILI RASIMU YA KATIBA KAMA INAVYOTAKIWA.

TAARIFA HIYO IMEONGEZA KUWA HALI HIYO IMEJITOKEZA KUPITIA BAADHI YA WATUMISHI WAKUU SEREKALI AMBAO NI WAKRISTO KUSIKIKA WAKISEMA NDANI NA NJE YA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAKITAHADHARISHA KUWA MFUMO WA SEREKALI TATU ULIOPENDEKEZWA NA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KUWA UTASABABISHA ZANZIBAR KUWA NA SEREKALI YAKIISLAM MADAI AMBAYO SI SAHIHI.

HATA HIVYO TAARIFA HIYO IMEFAFANUA KUWA INAVYOONEKANA NI KWAMBA BAADHI YA WAJUMBE WA BUNGE HILO WANATETEA MFUMO WA SEREKALI MBILI SI KUTOKANA NA MADAI YAKUIMARISHA MUUNGANO BALI NIKUSIMAMIA AJENDA YA KANISA YAKUIDHIBITI ZANZIBAR.

AIDHA BARAZA HILO LIMESEMA KUWA AJENDA HIYO NDIO ILIYOWASUKUMA MAWAKALA WA KANISA KUTUMIA NGUVU ZAO KUISHINDIKIZA ZANZIBAR KUJITOA KATIKA JUMUIYA YA NCHI ZA KIISLAM OIC KWA MADAI KUWA HAINA MAMLAKA YAKUJIUNGA NA INAYOPASWA KUFANYA HIVYO NI SEREKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAMBO AMBALO HALIJAFANYIKA HADI SASA NA BADALA YAKE IMEFUNGUA UBALOZI WA VATICAN NCHINI.

TAARIFA HIYO IMEELEZEA MASIKITIKO YA WAISLAM KUONA KUWA VIONGOZI WAKUU WA NCHI KUTOWAKEMEA MAWAKALA WA KANISA ZINAZIHATARISHA AMANI YA NCHI NAKUTOKEA MSUKOSUKO WA MUUNGANO.

BATAKI IMESEMA KUWA HATUA ILIYOFIKIWA NCHINI YAKULAZIMISHA KUFUATWA MATAKWA YA KANISA NDANI YA VYOMBO VYAKUTUNGA SHERIA LIKIWEMO BUNGE MAALUM LA KATIBA INAWEZA KUAMSHA HISIA KALI ZA KIDINI KWA WAISLAM WA ZANZIBAR KUONA KUWA KUNA UADUI NA NJAMA ZILIZOPANGWA DHIDI YA DINI YAO NA NCHI YAO.

BARAZA HILO LIMEELEZEA KUSKITISHWA KWAKE NA KITENDO CHA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA CHA KUWAFUATA MUFTI WA TANZANIA SHEIKH ISSA SHAABAN SIMBA NA POLYCAP KARDINAL PENGO WA KANISA KATOLIKI NA KUFANYA NAO MAZUNGUMZO BILA YAKUMSHIRIKISHA MUFTI MKUU WA ZANZIBAR INAASHIRIA UBAGUZI NAKUWADHALILISHA WANANCHI WA ZANZIBAR.
 
TAARIFA YA BARAZA HILO IMEWATAKA WAISLAM WA ZANZIBAR KUILINDA DINI YAO,KUPUUZA TOFAUTI ZAO ZA KISIASA NA MISIMAMO YA KULINDA SERA ZA VYAMA VYAO NA BADALA YAKE KUITIKIA WITO WA MOLA WAO WA KUSHIKAMANA PAMOJA BILA YAKUFARAKANA NA KUILINDA NCHI YAO KWA GHARAMA YOYOTE.

0 comments:

Post a Comment