Baadhi ya watu waliohuhudia ajali.
Watu kadhaa ambao walikuwa wanasafiria
treni ya jioni jijini Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya treni hiyo
kugongwa na lori.
Tukio hilo
lilitokea jana katika eneo la Tazara Buguruni lililopo Manispaa ya Ilala,
wakati treni hiyo ya saa 12 jioni ilipokuwa inatokea katikati ya Jiji la Dar es
Salaam (Stesheni ya Treni) kuelekea eneo la Ubungo Maziwa jijini humo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walieleza kuwa, ajali
hiyo ilitokea baada ya lori namba T 124 ATG aina ya Toyota Scania ambalo
lilikuwa limeegeshwa katikati ya reli kuigonga treni, hivyo kusababisha safari
za treni kuishia hapo.
"Watanzania tumekosa ustaarabu kabisa, kila siku
tunajua wazi kuwa hii reli huwa inatumika na treni, lakini leo (jana) unamkuta
mtu ameegesha gari katikati ya reli. Tunaiomba Serikali iweke sheria kali za
kuwabana hawa watu wazembe wanaotaka kuua mamia ya watu," alisema Mkazi wa
Buguruni aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mussa.
Usafiri huo wa treni maarufu kwa jina la Treni ya Mwakyembe ulizinduliwa
rasmi na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe mwishoni mwa mwaka jana
ambapo lengo ni kuhakikisha inahudumia wananchi kwa gharama nafuu jijini
0 comments:
Post a Comment