Ukumbusho wa:-
Kujizuia Kukata Kucha na Nywele Kwa Mwenye Kutia Nia Ya Kuchinja,
Kuhusu Takbiyrah Siku Za Dhul-Hijjah
Tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu mambo mawili muhimu tunayoghafilika nayo katika masiku ya Dhul-Hijjah
1-Kuhusu
Kuchinja: Wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa, wanatakiwa
wajizuie kukata nywele na kucha kuanzia unapoingia tu mwezi wa
Dhul-Hijjah mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni
maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:
عن
أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (ِذَا
رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ،
فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ) وفي راوية: (فَلَا يَأْخُذْ مِنْ شَعْرِهِ وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا ، حَتَّى يُضَحِّيَ) مسلم
Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)
Na katika riwaya nyingine (Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja) [Muslim na wengineo]
Hii ni fadhila na neema kwetu maana tunakuwa katika hali ya 'Ihraam' kama waliokuwa kwenye Hijjah.
Ikiwa amesahau mtu, mfano akakata kucha basi aendelee tu na nia yake mpaka amalize kuchinja.
Kila
mwenye uwezo wa kuchinja anawajibika kutekeleza ‘amali hii tukufu.
Vile
vile ikiwa mtu hakuweka nia tokea mwanzo wa mwezi ya kuchinja anaweza
kutia nia siku za mbele au hata akaamua kuchinja siku yenyewe ya Yawmun-Nahr
(siku ya kuchinja) ambayo ni siku ya kwanza 'Iyd baada ya Swalah na
sio kabla ya Swalah.
Na imeruhusiwa kutoka siku hiyo au ya pili ya 'Iyd
au kuchelewesha hadi siku ya mwisho ya Ayyaamut-tashriyq (siku za Tashriyq) ambayo ni siku ya kumi na tatu Dhul-Hijjah.
2- Kuleta Takbiyrah kuanzia tarehe 1 Dhul-Hijjah mpaka Tarehe 13 Dhul-Hijjah kama ifuatavyo:
Takbiyr hii ni aina mbili:
i) Takbiyratul-Mutwlaq - Za Nyakati Zote
Takbiyr
wakati wote usiku au mchana tokea Magharibi unapoingia tu mwezi wa
Dhul-Hijjah na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13
Dhul-Hijjah) inapoingia magharibi.
ii)Takbiyratul-Muqayyid - Za Nyakati Maalumu
Takbiyr baada ya kila Swalah na huanza asubuhi ya siku ya 'Arafah mpaka inapoingia magharibi ya siku ya mwisho ya Tashriyq.
Inavyopasa kufanya Takbiyrah baada ya kutoa salaam ni hivi:
الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد
"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Walillahil-hamd .
Makala haya ni kwa hisani kubwa ya Al Hidaya;
Munira blog inawatakiwa wasafiri wote waliosafiri na wanao safiri kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hijja,salama na amani,na iwe Hijja yao HIJJA MABRUURAH
HAWA NI WATU WALIOFURIKA WAKATI WA HIJJA.
0 comments:
Post a Comment