Rais mstaafu awamu ya pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Al haj Ally Hassan Mwinyi,amewaaga Mahujaji.
Hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Tanzania Muslim Hajj Trust imefanyika hivi punde katika ukumbi wa Starlight Hotel uliopo jijini Dar es salaam.
Akitoa
nasaha zake kwa waumini waliohudhuria maagano hayo,mzee mwinyi alisema
ibada ya hija ni ibada inayoambatana na bahati kutoka kwa Mwenyezi Mungu,hivyo unavyoipata nafasi hiyo unatakiwa uitumie kwa ufanisi zaidi.
"Ndugu
zangu mahujaji,nawapeni hongera,lakini kuhiji ni bahati,ndiyo maana
wengi wetu tunahiji tukiwa ni wazee,bila shaka katika ujana wetu
tulikuwa tuna nia ya kwenda kuhiji lakini,hatukujaaliwa,na sasa bahati
imetuangukia,basi tuitumie vizuri"Alisema.
Aliendelea kusema kwamba,"Tunachotaraji
baada ya kurudi kwenu ni kuondokewa na madhambi,sasa ukitaka
kuyarudisha hayo madhambi kidogo kidogo hiyo ni shauri yako",mwisho wa kumnukuu.
Awali
akiongea katika hafla hiyo,katibu mkuu wa Tanzania Muslim Hajj Trust
Al haj Abdallah Jabir aliwatahadharisha mahujaji muda wote wa safari kuwa makini na ukarimu
watakaopewa na watu wasiowajuwa.
"Tumepokea
barua kutoka Serikali ya Saud Arabia kwamba kuna baadhi ya watu wa Asia,wanawakarimu mahujaji kwa vinywaji vikiwa vina madawa ya kulevya na
baada ya kupatwa na usingizi wanawaibia kila kitu",alisema.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa manispaa ya Mtwara Mikindani Sheikh Suleyman Ahmad Mtalika alisema,"Hadi
sasa sijaamini kama nami ni mmoja wa mahujaji,kwani ni azma ambayo
nilikuwa nayo muda mrefu sana,namuomba Mungu anipe afya njema ili
nikaifanye Ibada ya Hijja kikamilifu hatimaye nikirudi nitoe muongozo
mwema kwa familia yangu".
Naye Ustaadh Abdu Shakuor Maulid wa Madrasat Qadiriyyah kutoka Dodoma mjini,akiongea na Munira blog amesema "Kwa kuwa ni mara yangu ya pili,nataraji ibada hii nitaaifanya vizuri zaidi,kwani mara ya kwanza nilikuwa ni mgeni wa mambo mengi"mwisho wa kumnukuu.
Taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust itawasafirisha
mahujaji wake kwa makundi mawili,ambapo kundi la kwanza linaondoka saa
tisa usiku wa leo na kundi la pili litaondoka usiku wa kuamkia tarehe 7
october.
Munira blog inawatakia safari njema na Hijja mabruor.
Munira blog inawatakia safari njema na Hijja mabruor.
HAPA WAUMINI WANASOMA DUA KWA AJILI YA KUANZA HAFLA YA KUWAAGA MAHUJAJI.
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALLY HASSAN MWINYI AKIHUTUBIA LEO KATIKA UKUMBI WA STARLIGHT HOTEL.
KATIBU MKUU WA TANZANIA MUSLIM HAJJ TRUST SHEIKH ABDALLAH JABIR AKIZUNGUMZA.
BAADHI YA AKINA MAMA AMBAO NAO NI MIONGONI MWA MAHUJAJI WAKIWA KATIKA HAFLA FUPI YA KUAGWA.
USTAADH ABDUSHAKUOR KUTOKA DODOMA
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MTWARA MJINI SULEIMAN AHMAD MTALIKA,WAKATI AKIONGEA NA MUNIRA BLOG
0 comments:
Post a Comment