Mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Morogoro jana iliyatupa maombi ya Sheikh Ponda Issa Ponda.
Akizungumza katika mahakama hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Kabateamesema maombi ya wakili Juma Nassor kwa niaba ya mteja wake hayana msingi hivyo Kesi hiyo imeamuriwa kubaki mkoani Morogoro.
Awali mawakili upande wa mshitakiwa wakiongozwa na Juma
Nassor waliiomba mahakama kwamba shitaka la kwanza la linalomkabili mteja wao la kukiuka masharti ya kifungo cha nje iliyotolewa na mahakama ya kisutu,ikasikilizwe katika mahakama hiyo na hivyo kuiomba ihamishwe kutoka morogoro.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi
wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.
0 comments:
Post a Comment