Makhatwibu katika Misikiti mbalimbali nchini wametakiwa kutokuwadhulumu waumini wao..
Rai hiyo imetolewa na Sheikh Suleiman Amran kilemile alipokuwa anawasilisha mada ya umuhimu na nafasi ya Lugha ya Kiarabu kwa Waislamu.
Amesema ni muhimu sana kwa waislamu kujifunza Lugha ya Kiarabu,kwani licha ya kuwa ni Lugha ya Mawasiliano lakini pia inasaidia kurahisisha kulifikia lengo la kusoma kwa muda mfupi,
Aliendelea kuwaambia licha ya umuhimu huo,lakini ni wazi kabisa waislamu wengi hawajifundishi na hawaijuwi Lugha ya Kiarabu.
"Ndugu washiriki wa semina hii,pamoja na udhaifu huo,lakini bado makhatwibu wetu wanaendelea kutoa khutba kwa kutumia kugha ya kiarabu,kufanya hivi ni kuwadhulumu waumini."alisema.
Sheikh Kilemile aliongeza kwa kusema"kutoa khutba kwa lugha ambayo waumini hawaifahamu ni kuwanyima haki yao ya msingi,ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu aliwatuma Mijumbe kwa Mujibu wa Lugha zao",mwisho wa kumnukuu.
Semina hiyo iliyowahusiha maimamu,makhatwibu na waalimu wa madrasa iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita,ilifanyika katika ukumbi wa Jaafar Complex chini ya uandalizi wa World Islamic Call Society.
0 comments:
Post a Comment