Mzazi mmoja amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieth Mnangi, alisema jana kuwa mzazi huyo, Lewana Melkiory (38) mkazi wa Sinza, alijirusha kutoka wodi ya wazazi ghorofa ya pili juzi usiku na kufariki dunia papo hapo.
Alisema mwanamke huyo alijifungua Oktoba Mosi na kulazwa hospitalini hapo na mtoto wake.
Kamanda Marieth alisema sababu za kujirusha kwa mwanamke huyo hazijafahamika, na maiti imehifadhiwa hospitalini hapo.
0 comments:
Post a Comment