Sep 13, 2013

Sheikh wa UHAMSHO mahututi.


Sheikh Azzan Hamdan mmoja katika viongozi wa Taasisi ya Uhamsho Visiwani Zanzibar amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na inaelezwa kuwa ana hali mbaya.

Kwa mujibu wa ripota wetu kutoka Zanzibar Ustaadh Shukran Muhammad katika mawasiliano kwa njia ya simu jana usiku,anasema Sheikh Azzan alifikishwa Hospitalini hapo jana (juzi) na kulazwa wodini lakini leo hii (jana) kutokana na hali yake kuwa mbaya amehamishiwa wodi maalum kwa ajili ya matibabu zaidi alisema.

Aliendelea kusema kwamba kimsingi Shekh Azzan afya yake si mzuri na ndiyo maana ana utaratibu wa kwenda India kupata matibabu maalumu kila baada ya miezi sita,lakini tokea wamkamate na kumweka ndani wamemzuwia kwenda India sasa hii imezidisha kuwa hali tete,cha msingi ALLAAH amnusuru lakini kama hali itakuwa mbaya zaidi basi lawama itaiangukia serikali.

Wakati huo huo hukumu ya kesi ya viongozi wa Uhamsho inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi huu.
 USTAADH SHUKRAN MUHAMMAD

0 comments:

Post a Comment