Jan 1, 2014

Misri kuzuia mali za viongozi wa Ikhwanul Muslimin

Serikali ya Misri imetoa amri ya kuzuiwa mali za mamia ya viongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchini humo kama sehemu ya hatua za ukandamizaji zinazotekelezwa dhidi ya kundi hilo na serikali ya mpito ya nchi hiyo inayoungwa mkono na jeshi. 

Abdulazim al Shiri msemaji wa Wizara ya Sheria ya Misri ameeleza kuwa    kamati ya wizara hiyo inayohusika na hesabu za mali imeagiza kuzuiwa mali zinazohamishika na zisizohamishika za viongozi 572 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.

Viongozi wa Ikhwani waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Muhammad Morsi Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na familia yake, viongozi wa majimbo wa harakati hiyo na wajumbe wa idara kuu ya miongozo ya harakati hiyo. 

Mbali na hao, Azza el Garf ni mwanachama mwingine mwanamke wa Ikhwani anayeonekana katika orodha hiyo pamoja na mke  na binti wa Khairat Shatir, afisa wa ngazi ya juu wa Ikhwanul Muslimin aliyeko jela.

0 comments:

Post a Comment