Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono
maarufu kama ‘dada poa’ usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye
operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya
jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.
Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye
Manispaa ya Kinondoni na Ilala ambapo baadaye walihifadhiwa kwenye
Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) kabla ya
kufikishwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa makosa ya uzurulaji.
Ombaomba hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo
walitakiwa kurudi katika makazi yao kuanzia leo ili wasichukuliwe hatua
za kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick
alipohojiwa alisema,operesheni hiyo,imebaini zaidi ya asilimia 70
wanatoka mikoani .
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kukamatwa kwa ombaomba hao na
kueleza kuwa zoezi hilo ni endelevu.
0 comments:
Post a Comment