KIWANJA CHA CHA NG'OMBE NI MALI YA WAISLAM.
- KILINUNULIWA NA RAIS WA MISRI.
- LENGO NI KUJENGA CHUO KIKUU CHA KIISLAM AFRIKA
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Sheikh Abdallah Muhamed kutoka Tarime mkoa wa mara alipokua anawasilisha salamu maalum kutoka mkoa huo kwa waislamu waliohudhuria kongamano hilo lililofanyika katka ukumbi wa Diomond Jubilee na kuwashirikisha wa waislam wa mikoa mbalimbali.
Alisema katika uhai wa aliyekuwa rais wa misri enzi hizo marehemu Abdul nassir,aliununua uwanja huo chang'ombe kwa thamani ya milioni mbili (kwa wakati huo) kupitia Bank ya Othman iliyokuwepo katikati ya mji wa Dar es salaam.
Aliendelea kuujuza umma uliofurika ya kwamba taasisi ya waislamu enzi hizo EAMWS ndiyo iliyopewa dhamana ya kuumiliki na kuuendeleza uwanja huo.
Aliwataja baadhi ya viongozi wa EAMWS kuwa ni Mar hum sheikh Said Tewa ambaye alikuwa ni mwenyekiti,Mar hum sheikh Azan ambaye alikuwa katibu mkuu na Mar hum sheikh Omar Muhaji ambaye alikuwa mshika pesa ndiyo waliokuwa wawakilishi wa waislamu kupitia taasisi hyo.
lengo kuu la rais wa misr hayati Adbul Aassir ni kujenga chuo kikuu cha kiislam cha Afrika mashariki,alisema sheikh Abdallah Muhamad ambaye alijinadi kuwa ni mkurya wa kwanza kuwa muislam hapa Tanzania.
Aliwafahamisha waislamu hao kwamba baada ya utawala wa Tanzania kwa wakati huo kuona kwamba waislamu watakua na kishindo katika hili,ndipo ikafanywa njama ya kuivunja taasisi hiyo iliyokuwa inategemewa na waislamu wengi na kuundwa chombo ambacho kina maafa na madhara kwa waislamu bila ya kukitaja chombo hicho wala kuyafafanua maafa hayo.
Alisema baada ya kuanzishwa kwa chombo hicho ambapo amedai kilianzishwa kwa msukumo na nguvu ya kanisa ndipo uuzaji wa kiwanja hicho kidogo kidogo ulipoanza.
"Naawaambieni ndugu zangu waislaum,mar hum Abdul Nassir aliwanunulia waislamu wa Tanzania uwanja mkubwa sana,lakini muuzaji hakuwashirikisha waislamu hata kidogo,kwa misingi hiyo sisi waislamu hatutambuwi kuuzwa kwa uwanja wetu,na ninatoa wito tusiogope kupigania haki yetu mpaka tuone tunarudishiwa mali yetu" mwisho wa kunukuu.
Mara baada ya kuwasalimia waislamu waliofurika kusikiliza tamko la waislam juu ya kusudio la serikali la kufuta mitihani ya somo la dini mashuleni,sheikh Abdallaah Muhammed alisema yeye ndiye mjumbe pekee wa iliyokuwa EAMWS ambaye mpaka leo yupo hai kwa hiyo anayajuwa mengi yaliyofichwa chini ya zulia.
Sheikh Abdallah Muhamed akiwajuza waislamu (asili ya kupatika kiwanja cha chang'ombe) waliofurika katika kongamano lilifanyika katika ukumbi wa Diomond Jubilee mwishoni mwa wiki iliyopita.
Picha na habari ni kwa mujibu wa mwandishi wetu wa muniramadrasa.blogspot
Masheikh (viongozi wa waislam) wakinyanyua mikono yao juu kuashiria umaoja na mshikamano.
Masheikh wakimsikliza sheikh Abdallah Muhamed alipokuwa akidadavua asili ya kupatikana uwanja wa chan'gombe ambao umeuzwa kwa madai ya bila ya kuwashirikisha waislamu.
Sheikh Abdallah Muhamed akisisiiza jambo kwa waislamu.
0 comments:
Post a Comment