Aug 19, 2013

WANANCHI PINGENI TABIA YA POLISI KUUWA HOVYO PROF.LIPUMBA;


  • POLISI WANAFANYA UNYAMA                                                                                      
     
    Na mwandishi wetu wa munira;                            
    Watanzania wametakiwa kujitokeza na kupinga hadharani tabia inayoota mizizi ya jeshi la polisi la kuwapiga risasi na kuwakamata hovyo viongozi wa dini na wa vyama vya siasa pindi wanapotumia fursa ya kusema ukweli.

Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema “Chama changu kina laani matukio ya Jeshi la Polisi ya kutumia nguvu kupita kiasi na kuwapiga risasi viongozi wa dini na viongozi wa siasa pale wanapotimiza wajibu wao kwa waumini wao ,kwa mfano tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda kisha kuondolewa kwa nguvu muhimbili kabla hajapona,hiki ni kitendo cha kinyama ambacho imefika wakati Watanzania ni lazima wajitokeze hadharani kupinga  unyama huo kwa nguvu zote kwani tabia hii inaonekana kukomaa”,mwisho wa kumnukuu.

Katika nchi yenye Demokrasia ya kweli,na nchi inayodai inaongoza kwa utawala bora wa sheria ni aibu sana kuruhusu jeshi lake kufanya unyama wa aina hii,alisema
 MWNENYEKITI WA CHAMA CHA (WANANCHI CUF)AKILAANI TUKIO LA KUPIGWA RISASI NA KUTOLEWA HOSPITALINI KABLA HAJAPONA SHEIKH PONDA.


















HAPA SHEIKH PONDA AKIWA CHINI YA ULINZI WA MAASKARI KANZU AKITOKA WODINI (MOI) KUELEKEA SEGEREA.























IGP SAID MWEMA AMBAYE ASKARI WAKE WANATUHUMIWA KUMPIGA RISASI SHEIKH PONDA.