·
SERIKALI YAAMBIWA
IJIANDAE KUTUMALIZA,LAKINI UKWELI TUTASEMA TU.
·
UPENDELEO KWA
WAKRISTO WAANIKWA.
Waislamu
wamefahamishwa sababu zilizopekea Sheikh Ponda Issa Ponda kupigwa risasi hivi
karibuni.
Hayo yaliwekwa
wazi na Sheikh Suleyman Daud alipokuwa anawasilisha mada ya KWA NINI SHEIKH
PONDA KAPIGWA RISASI.
Ameyasema hayo leo
jioni katika viwanja vya Mwembe Yanga wakati Waislamu walipofurika kwa ajili ya
kusikiliza tamko la Waislamu juu ya kadhia hiyo.
"Sheikh Ponda
hakuwahi kuchochea bali Sheikh Ponda alikuwa anawasilisha madai ya Waislamu kwa Serikali na kuwajulisha Waislamu juu ya dhulma wanazofanyiwa kutoka kwa
watawala wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,
Sheikh Suleyman
alibainisha madai hayo kuwa ni pamoja na Serikali kufanya upendeleo wa makusudi kwa Wakristo kwa kuyapatia mabilioni ya shilingi makanisa yote nchini kwa
kila mwaka chini ya Memorandum of Understanding (MOU) ambao ulisainiwa mwaka
1992 ambapo Edward Lowasa alisaini kwa niaba ya Serikali.
Leo wakristo wana Mashule makubwa makubwa,wana Hospitali kubwa kubwa ni kwa sababu ya mapesa hayo
ambayo sisi Waislamu ni sehemu ya walipa kodi.
Mbali ya hayo Sheikh Ponda amekuwa anakumbusha madai ya mauaji yaliyofanywa na polisi katika
msikiti wa Mwembe Chai mwaka 1998 na Serikali hii hii kukataa kuunda tume wala
kuwafikisha mahakamani wauwaji huku ikiunda tume ya kuchunguza mauaji ya mbwa
yaliyofanywa na raia wa kigeni baada ya mbwa huyo kupewa jina la Immagration.
Aliendelea kusema
kwamba Sheikh Ponda amekuwa anadai haki ya mtoto Chuki Athman aliyepigwa risasi
kwa madai kakutwa na nyaraka za uchochezi,huku akihoji kama hiyo ni hukumu
sahihi kwa mwenye kukutwa na kitu kama
hicho.mtoto huyo hadi leo amepooza mwili.
Mwaka 2001 Imamu
akitoka katika Swala ya ijumaa kule Zanzibar alipigwa risasi mbele ya msikiti kwa madai
kwamba yeye alikuwa ni mmoja wa waliohamasiha maandano ya chama cha siasa
ambayo yalikuwa yafanyike siku inayofuata.
Aidha Sheikh Suleyman alisema Sheikh Ponda alikuwa anaikumbusha Serikali mara kwa mara juu
ya madai ya Waislamu juu ya dhulma na ukandamizwaji unao fanywa na Serikali hii
ambapo mwaka 1989 Halmashauri kuu ya Waislamu iliyafikisha madai hayo kwa Rais
wa wakati huo (Mkapa) ambapo yeye alijibu kwamba yeye pia ni rais wa wala
nguruwe lakini baada ya miaka kumi (kwa maana mwaka 2009) madai hayo hayo
tukayachapa katika kitabu na kuyafikisha katika idara zote za serikali kuanzia
ngazi ya rais hadi ngazi ya chini (Mkuu wa wilya Tanzania mzima) lakini hadi leo serikali inajifanya kiziwi na inapokumbushwa mkumbushaji anaitwa mchochezi.
Pomda alikuwa
anawauliza iweje waislamu waliobambikiwa kesi ya kuchoma kanisa pale Mbagala
wamewekwa ndani hadi leo na wamenyimwa dhamana lakini wakristo waliochoma
msikiti kule Tunduma hawajakamwa na hata vyombo vya habari havikuripoti,haki na
uadilifu uko wapi.
Mbali ya hayo kuna
dhulma lukuki katika Sekta ya Elimu na Ajira,haya ndiyo ambayo Sheikh Ponda akiyasema
nasi tutayasema daima.
Sasa kwa madai
hayo ndipo Serikali hii ikaona eti Ponda ni mchochezi ndipo wakaona wampige
risasi wakiamini kwamba watafunga midomo ya waislamu,tunaomba wajuwe
wanajidanganya,hata Sheikh Ponda akifa lakini madai yetu bado yapo pale pale.
"Ikiwa Sheikh Ponda
anapigwa risasi kwa madai ya wazi kabisa,mbona maaskofu wametoa waraka wa
kumkashifu Rais Kikwete na hawajakamatwa wala kupigwa risasi,mbona kuna
viongozi wa vyama vya siasa wamesema watahakikisha nchi haitaliki na wanafanya vurugu kila kukicha bila kukamatwa
wala kupigwa risasi,naomba Serikali ifahamu kwamba amani pasipo kutenda haki ni
sawa na kiini macho,na kwa kasi hii wanayotupeleka,wajuwe kwamba itafika hatua hali itakuwa
mbaya kwetu sisi na kwao wao,kwani tutakaposema basi kuonewa kwetu itakuwa bora kufa kuliko kuishi".alisema
“Naomba Serikali ifahamu kwamba kama wao wataona kwetu sisi waislamu kufa kwetu ni lazima kwa sababu ya kuzungumza bayana dhulma munazotufanyia,basi
jiandaeni kutumaliza sote,lakin katu hatutonyamaza”,mwisho wa kumnukuu.
HUU NI UMMA WA WAISLAMU WALIOFURIKA LEO HII KATIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA JIJINI DAR ES SALAAM.