Polisi nchini Kenya
wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje
ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi hichi kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile
kilikuwa na mikono miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandikwa ''Kavuludi wewe
ndiye utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia
marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na
tukio hilo na
kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo
inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu
nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.