Pichani
ni walinzi wa Amani wakiwa katika moja ya doria kwenye mitaa ya mji wa
Goma, mwanzoni mwa wiki hii kumetokea mapingano katika eneo la vilima
vya Kibati Magharibi ya Kivu ambapo kundi la waasi la M23 lilishambulia
walinzi wa amani wa Misheni ya Kutuliza Amani katika DRC ( MONUSCO)
waliokuwa katika Operesheni ya kulinda raia wakishirikiana na Majeshi ya
Serikali ya DRC. Shambulio hilo limesababisha mwanajeshi Mtanzania
kupoteza maisha na wengine 10 wakiwamo wanajeshi wa Afrika ya Kusini
wamejeruhiwa.
Tukio la kushambuliwa kwa walinzi hao limelaaniwa vikali
na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa
Mataifa. Ban Ki Moon na Baraza Kuu wametuma salamu za rambirambi kwa
familia ya marehemu na familia za wale waliojeruhiwa na kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika ya Kusini. Aidha
Baraza Kuu limesisitiza kwamba vitendo vinavyolenga kudhoofisha mamlaka
ya MONUSCO havitavumiliwa.
Na Mwandishi Maalum
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amelaani kuuawa kwa Mlinzi wa
Amani kutoka Tanzania ambapo wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya
kushambuliwa na kundi la waasi la M23 katika katika eneo la Mashariki ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaii wa Katibu Mkuu , inaeleza
kwamba. “ Katibu Mkuu analaani kwa nguvu zote mauaji ya mlinzi huyo na
kujeruhiwa kwa walinzi wengine 10 na anatoa salamu zake za rambirambi
kwa familia za walinzi hao na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Afrika ya kusini”.
Mashambulizi
dhidi ya walinzi hao wa Amani yametokea siku ya jumatano katika Vilima
vya Kibati Magharibi ya Kivu ambako Misheni ya kutuliza Amani ya Umoja
wa Mataifa katika DRC ( MONUSCO) ilikuwa ikisaidiana na majeshi ya
serikali ya DRC kuwalinda raia katika eneo la Goma ambalo lina idadi
kubwa ya watu.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, MONUSCO ilijibu mashambulizi hayo kwa kutumia
zana mbalimbali za kivita yakiwamo makombora, mizinga na helkopta za
kivita wakati majeshi ya DRC yalitumia askari wa ardhini, vifaru na
helkopta za kivita na kwamba operesheni hiyo bado inaendelea.
Taarifa
inaeleza zaidi kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuwajibika na
kuhakikisha inachukua hatua zote muhimu kwa kuzingatia Azimio namba 2094
( 2013) la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo
linasisitiza ulinzi wa raia katika eneo hilo la Mashariki ya Kongo.
Wakati
huo huo , wakati mapigano yakiendelea, Baraza Kuu la Usalama la Umoja
wa Mataifa, katika kikao chake kilichofanyika siku ya Alhamisi nalo
limetoa tamko la kulaani vikali tukio la kuuawa kwa mlinzi wa Amani wa
Tanzania, na kutoa salamu zako za pole kwa serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na familia ya marehemu pamja na wale waliojeruhiwa.
Tamko
la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limetolewa taarifa hiyo
baada ya Baraza hilo kupokea taarifa rasmi iliyowasilishwa na Naibu Mkuu
wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, Bw. Edmond Mulet kuhusu
kinachoendelea katika DRC.
Baraza
pia limelaani kwa nvugu zote dhidi ya kujirudia rudia kwa matukio
yanayofanywa na M23 yanayolenga MONUSCO na rais yakuwalenga raia na
MONUSCO.
Na kwa
sababu hiyo Baraza Kuu la Usalama limetaka mamlaka ya DRC kuchunguza
tukio la kuuawa kwa mlinzi huyo wa Amani na kisha kuwafikisha mbele ya
sheria watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
Aidha
Baraza Kuu limerejea tena tamko lake la kuitaka M23 na makundi mengine
yenye silaha katika DRC kuacha aina zote za machafuko na kuweka chini
silaha zao. Na kwamba, halitasita kupitisha vikwazo vya nyongeza kwa
yeyeyote yule ambaye atabainika kujihusisha na fujo na machafuko na
kwamba vikwazo hivyo vitahusu pia silaha.
Aidha
wajumbe 15 wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeipongeza
MONUSCO kwa namna ambavyo imekuwa ikitekeleza mamlaka yake na hususani
ya kuwalinda raia na limeitaka na kuihimiza MONUSCO kuendelea na wajibu
wake huo huku lilikisisitiza kwamba Baraza Kuu la Usalama halitavumilia
kitendo chochote kinacholenga kudhoofisha mamlaka ya MONUSCO.
Vilevile
Baraza limeitaka Expanded Joint Verification Mechanism ( EJVM)
kuchunguza madai ya kuwapo kwa vitendo vya urushwaji wa makombora
kuelekea nchi ya jirani ya Rwanda
Katika
hatua nyingine , Muwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika DRC. Bw.
Martin Koble naye ameelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo la kuuawa
kwa mlinzi wa Amani wa Tanzania.
Akielezea
masikitiko yake, Bw. Martin Koble anasema, “ mlinzi huyo wa Amani
ameyatoa muhanga maisha yake ili kuwalinda wananchi wa Goma. Ninaungana
na familia ya marehemu na walinzi wenzake katika kombania yake katika
kipindi hiki cha majonzi na wakati mgumu”.
Katika
mwaka mmoja uliopita, kundi la waasi la M23 pamoja na makundi mengine
yenye silaha mara kwa mara yamekuwa yakipambana na Jeshi la Serikali ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( FARD). Ambapo Mwezi Novemba mwaka
jana kundi hilo la M23 lilichukua kwa muda mji wa Goma.