Makundi ya wanamgambo wa Kikristo wanaojulikana kwa Anti – Balaka
jana waliwashambulia wafuasi wa dini ya Kiislamu huko Bangui, mji mkuu
wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Kikosi cha Umoja wa Afrika kinacholinda amani nchini humo MISCA.
Msemaji wa MISCA amesema kuwa, wanamgambo wa kundi la Kikristo la Anti – Balaka jana walifanya operesheni ya nyumba hadi nyumba ya kuwasaka na hatimaye kuwauwa kwa akali Waislamu 60 mjini humo.
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita, Waislamu wasiopungua 1,000 wameuawa wakiwemo wanawake na watoto.
Wakati huohuo, Rwanda imetangaza kuwa tayari kupeleka jeshi lake nchini humo chini ya mwamvuli wa kikosi cha Umoja wa Afrika.
Hayo yamesemwa na Louise Mushikiwabo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Rwanda. Hata hivyo hakuweka wazi idadi ya wanajeshi watakaopelekwa nchini humo.
Wakati huohuo, Joseph Nzabamwita Msemaji wa Jeshi la Rwanda amesema kuwa,hivi karibuni jeshi litatangaza idadi ya wanajeshi watakaopelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:
Post a Comment