Dec 24, 2013

Watu 14 wapoteza maisha Misri


Waziri mkuu wa Misri Hazem el-Beblaoui akitangaza kwamba chama cha Udugu wa kislamu ni " kundi la kigaidi"

Shambulizi la vilipuzi liliyotokea mapema leo asubuhi kwenye jengo la polisi mjini Mansourah, kaskazini mwa Misri, limesababisha jengo hilo kuporomoka. Shambulizi hili limewauwa watu 14 na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa. 

Waziri mkuu wa Misri, ambae anatuhumu chama cha Udugu wa Kislamu kuhusika na shambulizi hilo, amekitangaza chama hicho kwamba ni " kundi la kigaidi ".

Shambulizi hilo lilitokea ndani ya gari ndogo mapema siku ya Jumanne na kutetemesha jengo hilo la polisi wa usalama katika mji wa Maansourah kaskazini mwa Misri na ambalo liliporomoka kutokana na mlipuko huo.

Kaimu Waziri Mkuu Hazem Beblawi amesema shambulizi hilo ni la kigaidi.

Mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama nchini humo yameongezeka katika siku za hivi karibuni tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mwezi Julai mwaka huu.

Hadi sasa hakuna kundi lilijitokeza kudai kutekeleza shambuzi hilo ambalo ni baya sana kuwahi kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.

Serikali nchini Misri inasema inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa waliotekeleza shambulio hilo wanajulikana na baadae wafunguliwe mashataka.

0 comments:

Post a Comment