Hatimaye siri ya kuongoza kwa kushika nafasi ya kwanza katika masomo kumi na nne ya mtihani ya kidato cha nne imejulikana.
Mshindi huyo ni Salim Said Salim ambaye ni mukhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Dyccc iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam.
Akiongea na Munira blog kwa njia ya simu muda mfupi uliopita,Salim Said Salim amesema siri ya mafanikio yake ni juhudi za makusudi na usikuvu wa wazazi wake.
"Ndugu mwandishi nikupe siri,kwanza kabisa ni juhudi zangu binafsi,tangu nianze kidato cha kwanza sijawahi kwenda tuition zaidi ya kupata elimu hii hapo hapo shuleni Dyccc".
Aliendelea kusema "pili
ni ushirikiano mwema baina yangu na walimu wangu na wazazi wangu,kwa
kweli wazazi wangu walikuwa ni wasikivu kwangu,haijawahi kutaka kitu
kwao kina chohusu shule wakapuuza,kwa kweli nawashukuru sana".
Akijibu swali la mwandishi wa munira blog aliyetaka kujuwa kama matokea hayo aliyatarajia,alisema,"Ndiyo
niliyatarajia kwani toka nianze kidato cha kwanza sijawahi kushika
nafasi yoyote zaidi ya kushika nafasi ya kwanza,unajuwa juhudi zako
mwenyewe unaziona,kilichobaki ni Qadari ya ALLAH"mwisho wa kumnukuu.
Mwishoni mwa wiki iliyopita yalifanyika mahafali ambapo kijana salim said salim aling'ara kwa kuwa mshindi wa jumla kwa kushika nafasi ya kwanza kwa masomo 14.
Hali hiyo iliwasukuma wajumbe wa bodi ya shule kuamua kumualika baba yake (salim) kuwa ni mmoja kati ya wageni rasmi.
Kwa sasa shule ya DYCCC ni moja katika shule zinazofanya vizuri huku majengo yake yakiwa yanavutia.
Mashaallah
ReplyDelete