Ripoti zinaeleza kuwa jamii ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imezingirwa huku vikosi vya Ufaransa na vinginevyo vikishindwa kuyapokonya silaha magenge ya Wakristo.
Abayomi Azikiwe mhariri wa Pan-African News Wire amesema katika mahojiano na waandishi habari kuwa, jamii ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati inazingirwa huku watu wanaojaribu kuondoka nchini humo wakizuiwa.
Hapo jana waasi wa Kikristo wa Anti Balaka waliwashambulia na kuwaua Waislamu watatu katika mji mkuu Bangui na inaripotiwa kuwa mashambulizi ya magenge ya Kikristo dhidi ya Waislamu yanashuhudiwa kila uchao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mhariri huyo wa Pan- African News Wire ametahadharisha kuwa, hali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itazidi kuwa mbaya, hadi pale mgogoro huo utakapotafutiwa suluhisho la kisiasa.
0 comments:
Post a Comment