WAISLAMU WAHIMIZWA KUOMBA DUA.
- DUA NI IBADA,
- TUYAONDOSHE MABALAA KWA KUOMBA DUA.
Waislamu wameshauriwa kukitumia kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kuomba Dua kwani Dua zao ndani ya kipindi hiki zinauhakika wa kujibiwa.
Hayo yapo ndani ya khutba ya Ijumaa ya kwanza ndani ya Ramadhani ya mwaka huu iliyosomwa leo hii katika msikiti wa Qiblatain uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam.
Akiitafsiri khutba hiyo kwa lugha ya Kiswahili Ustaadh Muhammad Khamis (imamu msaidizi) alisema hiki ni kipindi muhimu sana kumuomba ALLAH juu ya shida,mitihani na haja mbalimbali zinazotukabili sisi waislamu.
Amesema kwa "mujibu wa mafundisho ya Mtume S.A.W. ni kwamba Dua za watu aina tatu ni zenye kujibiwa,alimtaja mtu wa kwanza ni Mfungaji wakati anafuturu,mtu wa pili ni Msafiri na mtu watatu ni aliyedhulumiwa"mwisho wa kumnukuu.
Ndugu zangu Waislamu Mtume S.A.W anasema "Dua ni ibada,kwa kutumia dua,Nabii Ayyuob aliumwa kwa miaka mingi lakini alipona baada ya kumuomba sana ALLAH.vile vile nabii Nuuh naye alipata mtihani mzito wa kumezwa na samaki lakini alipata nusura baada ya kumuomba sana ALLAH,lakini pia Mitume kadhaa nao pia walipata taabu,shida na mashaka lakini kwa kumuomba ALLAH hatimaye ALLAH aliwapa nusra na faraja,hivyo basi na sisi tufanye wingi wa kumuomba ALLAH".
Aidha aliwakumbusha Waislamu juu masharti ya kuomba dua ikiwa ni pamoja muombaji awe na yakini kwamba Mwenyezi Mungu atamjibu,aidha muombaji amuombe mungu mara kwa mara,muombaji wakati anaomba dua ahakikishe kivazi chake,chakula chake na hata makazi yake ni ya halali.
USTAADH MUHAMMAD KHAMIS AKITAFSIR KHUTBA SWALA YA IJUMAA LEO KATIKA MSIKITI WA QIBLATAIN
0 comments:
Post a Comment