TUWEKEZE KATIKA MALEZI YA WATOTO WETU.
Na mwandishi wetu wa munirablog
Wazazi na walezi wa kiislamu wamenasihiwa
kuwekeza kwa hali na mali
katika malezi mema ya kiislamu kwani jamii inategemea malezi mema ili tuwe na
taifa lenye maadili mema.
Nasaha hizo zimesemwa leo hii na Shekh Yasir
Salim ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Elimu kwa wanafunzi wa
Madrasat Mus ab Bin Umayr iliyopo Sinza maeneo ya Sweat Conner jijini Dar es
salaam.
Sheikh Yasir ambaye ni katibu mkuu wa
HAY-ATUL ULAMAA alisema "jukumu la malezi ni letu sisi
viongozi wa familia na viongozi wa dini,hivvo tunatakiwa tuwekeze kwa hali na
mali ili tufikia malengo ya kuumbwa kwetu.
Akinukuu maneno ya Mtume S.A.W, Sheikh Yasir
alisema "Dinar (shilingi) iliyokuwa bora ni ile uliyoiwekeza katika
familia yako",akiamaanisha kutumia pesa yako kumuhudumia mtoto
wako katika nyanja ya elimu,afya,malazi n.k
Ndugu zangu tunatakiwa tuwekeze katika
malezi ya kiroho,kiakili na kimwili,billa ya hivyo hata ile dhana ya kuwa na
Madrasa bora kama hii itakuwa haina maana.
Kwa upande wake Sheikh Abdallaah Haruna
akiongea na Waislamu hao alisema imefika wakati tusione taabu kutumia gharama ili
tupate mafundisho au utaalamu wa watu wenye elimu bobezi.
Tumekuwa na utamaduni usiokuwa mzuri wa
kukubali kuwatumia waalimu au wataalamu wasiokuwa na umahiri au uwezo kwa
kukwepa gharama au kwa sababu zisizo kuwa na msingi matokeo yake kila kukicha tuna
zalisha wanafunzi au wataalmu wasio kuwa na sifa sahihi.
Aliendelea kusema kwa kutoa mfano,"hebu
ona wenzetu wa Marekani hawaangalii rangi wala Dhehebu,wana mchukua
Profesa Ibrahim Lipumba na kumpa vipindi kadhaa kufundisha huku wakimlipa kwa
gharama kubwa sana,wao wanaamini elimu bora ndiyo ufunguo sahihi wa maendeleo
ya kweli,sasa wakati wao wanawachukuwa wataallamu wetu sisi wenyewe
hatujishughulishi na hilo.aliwaasa waislamu kutoogopa gharama katika hilo."
Akiongea na blog ya munira
Bwana Yasin Shaaban Bakar ambae ni mzazi katika Madrasa hiyo alisema "juhudi
inayofanywa na madrasa hii ni kubw sana na inafaa kuungwa mkono,mwandishi wa
habari hebu tazama leo watoto wamesoma kwa uwezo mkubwa sana wamezungumza
historia ya Mtume S.A.W. na maswahaba kama kwamba wamewaona,hili ni jambo la
kuungwa mkono,sisi tumesoma enzi zetu tukatufundishwa Qur aan tena bila tafsir
lakini leo mtoto mdogo anafundishwa masomo tisa na anayamudu"mwisho wa
kumnukuu.
"kwa kweli elimu inayotolewa hapa
ni mzuri sana nafikiri mwandishi wa habari umeshuhudia namna mashindano
yalivyokwenda kila mtoto kaonyesha kuiva kimasomo,hata wale walioshindwa kujibu
baadhi ya maswali ni kutokana na woga sio kwamba hawajuwi,lakini kubwa
kinachotofautisha madrasa hii na madrasa nyengine ni kitu kimoja,madrasa nyingi
wanawahifadhisha masomo wanafunzi kwa ajili ya shughuli,lakini hawa wanasoma
kile ambacho wanafundishwa kwa mujibu wa mtaala wao",alisema i
Khadija Muhammad Said na kuungwa mkono na bi Asha Omar Rajabu ambao wote ni
wazazi.
kwa upande wake mtoto Yusuph Faisal (12)
ambaye ndiye mshindi wa kwanza katika Swaffu Rraabi'u( Darasa la nne) alisema
"kwa kweli nilikosa muda wa kujiandaa kutokana na kubanwa na masomo ya
shule (anasoma darasa la sita katika shule ya msingi luqman sinza palestina)
lakini nilifurahi sana baada ya kutangazwa kuwa nimeshinda,naamini mungu
amejibu dua yangu,kwani ustaadh wangu aliniambia niombe dua kabla ya kupanda
jukwaan",alisema.
mama mzazi wa mtoto huyo salma yusuf bakar
alionyesha wazi furaha yake baada ya kusema "kwa kweli furaha yangu
ni kubwa mno,sikutegemea hata kidogo,kwani mwaka jana alikuwa mshindi wa
tano,sikutegemea kwa kuwa kwanza mwanangu ni mtundu sana lakini pia tuition
(masomo ya ziada) zinambana sana kwa weli walimu wamefanya kazi kubwa sana,nina
ahidi kumuendeleza Inshaa Allah.
KATIBU MKUU WA TAASISI YA HAY-ATUL ULAMAA SHEIKH YASIR SALIM AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA ELIMU KWA WANAFUNZI WA MADRASAT MUS-AB BIN UMAYR,AKIONGEA NA WAISLAMU WALIOHUDHURIA TAMASHA HILO MUDA MFUPI BAADA YA KUGAWA ZAWADI KWA WASHINDI.
***********************************************************************************
PICHA NA MATUKIO YA TAMASHA LA ELIMU LA MADRASAT MUS-AB BIN UMAYR
ILI PICHA IPENDEZE,ILIMLAZIMU MGENI RASMI ACHUCHUMAE ILI ALINGANE KIMO NA MTOTO FATMA YAHYA RAMADHAN (MIAKA MITATU) AMBAYE NI MSHINDI WA KWANZA KATIKA DARSA LAKE LA JIM BAUN
HUYU NI MTOTO YUSUF FAISAL MSHINDI WA JUMLA AKIWA NA MAMA YAKE BI SALMA YUSUF FATAKI MUDA MFUPI BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI NA KUKABIDHIWA ZAWADI ZAKE.
HAWA NI WANAFUNZI WAKIFIKISHA UJUMBE KWA NJIA YA NGONJERA.
HAWA NI SEHEMU YA WAZAZI NA WANAFUNZI WALIOHUDHURIA TAMASHA LA ELIMU.
0 comments:
Post a Comment