SHEIKH BASSALEH.
- TUSIBAGUE ELIMU,
- KATIKA UISLAM HAKUNA U-KIHIYO
Imeelezwa ya kwamba katika zama zilizo pita waislamu waliutawala ulimwengu wote kutokanana wao kutobagua elimu.
Hayo
yamesemwa jioni hii na Imamu mkuu wa Msikiti wa Idrissa Sheikh Ally
Bassaleh (maarufu kwa jina la mzee wa kunukuu) alipokuwa akiwanasihi
wazazi na waislamu waliohudhuria katika Tamasha la Elimu kwa wanafunzi
wa Madrsat Mus-ab Bin Umayr ya Sinza Uzuri Manispaa ya Kinondoni Jijini
Dar esalaam.
Akinukuu maneno matukufu ya Mtume S.A.W. Sheikh Bassaleh alisema "Elimu ni Uhai wa Uislamu ndiyo maana Mtume akasema tena Elimu ni kama mnyama aliyekupotea,popote utakapo mkuta,basi mchukuwe" mwisho wa kumnukuu.
Aliendelea
kusema siri ya waislamu wa zama zilizopita ni kwamba wao hawakubagua
elimu gani wasome na elimu gani wasisome,ndiyo maana kwa utaratibu huo
waliweza kuutawala ulimwengu kwa kiasi kikubwa sana,lakini baada ya kuja
wakoloni wakaanza kutusambaratisha kidogo kidogo na kutunyang'anya
elimu hiyo na hatimaye kuwafanya baadhi ya wislamu kutilia mkazo elimu
ya dini pekee.
Akitoa mfano wa maneno na wa michoro alisema,"hili somo la hesabati (Aljebra) limeanzishwa na waislamu,walichokifanya upande wa pili niwao kutunyang'anya na kubadilisha kisha kuboresha namba kadha na kujifanya kwamba wao ndiyo wenyewe" huku akionyesha kwa michoro namba mbili na namba tatu za kiarabu namna zilivyogeuzwa na kuwa namba mbili na namba tatu za kizungu.
Sasa
ikiwa uislamu unahimiza kusoma pasipo kubagua elimu na ikiwa waislamu
wanaongozwa na Qur an ambayo imeitangulia sayansi kwa umbali mkubwa,basi
hakuna sababu ya sisi kutokusoma elimu nyengine.
"Leo
hao wapinzani wa uislamu wanakiri bayana kwamba Qur aan ni kitabu
chenye ukweli na elimu ya hali ya juu sana na kinaendana na sayansi
,sisi tuna waambia kwamba Qur aan ipo mbele ya Sayansi kwa masafa marefu
sana" alisema..
Alimtaja
mmoja wa mabingwa wa Sayansi Ulimwenguni Bwana Morris Bucayr ambaye ni
Mfaransa ya kwamba alikiri kupitia kitabu chake cha ukweli kuhusu
Bibilia,Qur aan na Sayansi.
katika hafla hiyo mgeni Rasmi alikuwa Sheikh Yassir Salim ambaye ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Tanzania (HAY-ATUL ULAMAA)
Madrasat Mus-ab Bin Umayr (ambayo inafanya vizuri sana katika nyanja ya elimu) ni moja katika madrasa zinazo simamiwa na kuendeshwa na taasisi ya DYCCC.
Hadi mwandishi wetu wa munirablog anaondoka katika Tamasha hilo bado lilikuwa linaendelea na tayari washindi walishatangazwa na kuzawadiwa,tuna ahidi kuwaletea habari na picha zaidi ya Tamasha hilo Inshaa Allaah
BAADHI YA WAZAZI WALIOHUDHURIA TAMASHA LA ELIMU LA MADRASAT MUS AB BIN UMAYR, HIVI PUNDE.
SHEIKH ALLY BASSALEH AKISISITIZA JAMBO.
HAWA NDIYO WAALIMU WA MADRASAT MUS- AB BIN UMAYR YA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment