- Zimezalisha masheikh wengi.
- Qur aan ingekuwa ijifafanuwe yenyew isingebebeka.
Na mwandishi wetu wa munirablog.
Waislamu nchini kupitia misikiti mbalimbali wametakiwa
kuzihuisha darsa za Mtume s.a.w. kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatekeleza
sunna ya mtume s.a.w.
Wito huo umetolewa jana baada ya Swala ya Maghrib na Sheikh
Suleyman Amran Kilemile alipokuwa ana zungumza na Waislam katika hafla fupi ya
kusheherekea kutimiza miaka kumi na tatu ya uwepo wa darsa ililoambatana na
shindano la Hadithi katika msikiti wa Kipata uliopo Kariakoo Jijini Dare s
salaam.
Alisema "Qur aan ingekuwa ijifafanuwe yenyewe pasipo kuwepo
kwa Hadithi (maneno ya Mtume s.a.w.) ni dhahiri isingechukulika.lakini
Mwenyeezi Mungu kwa Hekima zake akamfanya Mtume s.a.w. kuwa ni mtafsiri wa Qur
aan hiyo kupitia maneno yake'.
Alizinukuu Aya mbili (43 na 44) zilizopo katika Surat Nnahli
kuwa ni Aya zinazo thibitisha hilo
na kusema “wanaodai waishi na qur aan pekee hawa wanazipinga Aya hizi”
‘Kwa kipindi kirefu tulielekeza nguvu zetu kutafsiri Qur aan pekee
tukasahahu kwamba hadithi ndiyo sunna yenyewe lakini kwa masheikh wachache kama
hawa kuendesha Darsa za Hadithi kwa kweli wamefanya jambo la maana sana” alisema.
Alionesha masikitiko yake kwa baadhi ya misikiti kutokuwa na
Darsa mbalimbali zikiwemo za Hadithi na kumfanya atoe wito kwa maimamu na
masheikh mbalimbali kuzianzisha na kuzisimamia Darsa katika misikiti yao.
“Hizi darsa zinazo endeshwa baina ya maghrib na ishaa kwa kweli zimezalisha
masheikh wengi hapa bara na kule Zanzibar,tunapaswa kuziendeleza kwa zile
zilizopo na kuanzisha nyengine kwa misikiti ambayo haina darsa hizo tena
ikibidi hata waumini na viongozi wa misikiti wamwatafute masheikh wanye uwezo
wa kusomesha Darsa hizo”,mwasho wa kumnukuu.
Awali akitoa maelezo yake Mwalimu wa Darsa hiyo Sheikh Abdallah
Ahmad Bawazir alisema Darsa hiyo ameianzisha mwaka 2000 baada ya kuombwa na
viongozi wa msikiti huo ambao wengi wao wameshafariki.
“Tayari nimeshafundisha kitabu chote cha umdatul ahkaam,buluughul
maraam,na sasa tunaendelea na kitabu cha sunan abii daaud”Alisema
sheikh Bawazir.
Alieleza lengo la shindano hilo
ni kukuza na kuimarisha maarifa ya vijana ambapo vijana 18 (kati ya vijana 37
waliochukuwa fomu ) kutoka mikoa mbalimbali walishiriki Shindano hilo huku mshindi atakayepata
kwa asilimia mia moja akiahidiwa zawadi ya pesa taslim Shilingi laki tano
(500,000).
Kwa bahati mbaya hakupatikana mshindi kwa kujibu sawa sawa
kwa asilimia mia moja.
Pamoja na hivyo wadhamini wa Darsa hilo waliwazawadia washindi pesa taslim kwa
viwango tofauti kwa lengo la kuwahamasisha.
Washindi hao ni Abdallah Said Madijimba (Iringa),Abuu Hanifa
Said Bakar (Tanga),Abuu Muhammad Ahmad (Iringa),Hafswa Nassoro Ahmad (Dare s
salaam) na Omar Kulili (Dar es salaam).
Sheikh Abdalaah Bawaziri ni mahiri katika fani ya Hadithi na
kwa sasa ana miaka 35 tangua aanze kazi ya kufundisha Somo la Hadithi katika
misikiti mbalimbali hapa nchini.
Kwa sasa anaendesha Darsa za Hadithi katika misikiti ya Kipata
na Qiblatain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment