Jun 15, 2015

UISLAMU SI UGAID

Dunia imetakiwa kufahamu kwamba uislamu si ugaidi na ugaidi si uislamu.

Tanbihi hiyo imetolewa jana na Doctor sheikh Ahmad Totonji ambaye ni mwenyekiti wa INTERNATIONAL INSITUTE OF ISLAMIC THOUGHT ya Nchini Saudia Arabia.


 Akiongea katika kongamano la kuukaribisha mwezi wa Ramadhan lililoandaliwa na TAMPRO kwa udhamini mkubwa wa Amana Bank,Sheikh Totonji alisema kumekua na kasumba duniani ya kuwalisha imani watu ya kwamba Uislamu ni ugaidi,hii si sahihi,alisema.

Uislam ni dini ya Amani ,uislamu unapinga na kukemea mauaji,uislamu upo mbali kabisa na harakati zote zote za mauaji,alisema.

Akinukuu baadhi ya Aya mbalimbali kutoka katika Quraan tukufu,Sheikh Totonji alisema kwa mujibu wa hukumu ya Uislamu, kumuua mtu mmoja pasipo haki ni sawa na kuwaua watu wote.

Aidha sheikh Totonji ambaye alikua mgeni Rasmi ,alikanusha vikali madai ya kwamba magaidi ni waislamu kwa kusema "napenda ieleweke,uislamu si ugaidi na ugaidi si uislamu"mwisho wa kumnukuu.

Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu ya "Ndoa ni chanzo cha Utu wetu" lilifanyika jana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mamia ya waumini kutoka taasisi mbalimbali.







0 comments:

Post a Comment