Meya wa jiji la New York nchini
Marekani, Bill De Blasio, ametangaza kuwa shule zote za umma katika mji
huo zitakuwa zikifungwa kila mwaka wakati wa Sikukuu mbili muhimu za
Kiislamu za Idul-Fitr na Idul-Adh’ha.
Hatua hiyo inalenga kuonyesha
heshima kwa Sikukuu hizo mbili za Waislamu.
Meya De Blasio amesema
uongozi wa jiji la New York umeona pana haja ya kuweko na usawa katika
kutambua na kuheshimu shughuli muhimu za watu wa dini mbalimbali mjini
humo.
New York ina wanafunzi wasiopungua milioni 1.1 katika shule za
umma.
Majimbo kadhaa ya Marekani yakiwemo ya Massachusetts, Michigan and
New Jersey katika miaka ya hivi karibuni yameorodhesha sherehe za
Idul-Fitr na Idul-Adh’ha kwenye kalenda ya matukio kwenye shule zao.
Baadhi ya wachambuzi wanasema hatua hiyo
ni aina fulani ya mkakati wa kuwapumbaza Waislamu wa Marekani ambao
kwa hivi sasa wanakabiliwa na mashinikizo kutoka kwa vyombo vya usalama
na vya kijasusi vya nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
0 comments:
Post a Comment