Mar 16, 2015

AJALI YA KUTISHA SINGIDA

ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia
moja wamefariki dunia mkoani Singida leo,
baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina
ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina
ya Scania.

Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa
1.32 asubuhi katika barabara kuu ya
Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna
tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani
Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa
Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema
gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi
wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya
kuja Singida mjini.

Amesema hadi sasa miili ya abiria 10
wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na
miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa
na miili yote bado imehifadhiwa kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali
ya mkoa mjini Singida

0 comments:

Post a Comment