Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka viongozi wa
dini kutumia nafasi kukemea juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii kwa waumini wao na kuelimisha madhara yanayoweza kusababishwa na
teknolojia hiyo katika jamii.
Hatua hiyo ya TCRA imekuja kufuatia kukithiri kwa
vitendo vinavyoashiria kutumika vibaya kwa mitandao ya kijamii kama njia
ya mawasiliano hali inayochangia kuzidi kuporomoka kwa maadili.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma alisema
lengo la kukutana na viongozi hao ni kuwapa elimu kuhusiana na madhara
ambayo jamii inaweza kupata kufuatia ongezeko la matumizi mabaya ya
mitandao.
“Mitandao ni mizuri sana lakini tatizo ni jinsi
inavyotumika watu wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu tena bila kuwa na
hofu ya Mungu ndiyo maana tumerudi kwenu viongozi wa dini mtusaidie
katika hili:
Kwa kutumia nafasi zenu tuna imani mtawaelimisha
waumini ili waelewe kuwa kusambaza ujumbe unaoashiria uchochezi ni kosa
kisheria na inaweza kuwa dhambi kwani hakuna ambaye angependa amani
ivunjike”
0 comments:
Post a Comment