Feb 17, 2015

Kiongozi: Uislamu unafundisha kuamiliana vyema na watu


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu yanatuamrisha kuamiliana vyema, kwa insafu na uadilifu na wafuasi wa dini nyinginezo za mbinguni.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wabunge wa wafuasi wa dini za wachache katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu 'Bunge la Iran' mjini Tehran. 

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kile kinachoshuhudiwa leo hii huko Ulaya na Marekani ni njama na propaganda chafu zilizo dhidi ya Waislamu, na hivi sasa halizungumzwi suala la kwa nini Waislamu hawana  uhuru kamili katika nchi nyingi za Magharibi, bali  kinachoonekana sasa ni kwamba maisha ya Waislamu yamo hatarini. 

Kiongozi Muadhamu ameelezea hali bora ya wafuasi wa dini za wachache nchini Iran na kuwataka wabunge wa wafuasi hao kulinganisha miamala wanayofanyiwa hapa nchini na wafuasi wa dini za wachache katika maeneo mengine duniani. 

Ayatullahil Udhma Ali Khamenei amesisitiza kuwa, ulimwengu wa Kikristo unapasa kuelewa  thamani, heshima na matendo mema wanayofanyiwa wafuasi wa dini nyinginezo katika nchi za Kiislamu, mambo ambayo Wamagharibi hawayafanyi kwa Waislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametolea mfano wa jinsi jamii ya Wamagharibi inavyowakandamiza na kuamiliana vibaya na Waislamu na kusisitiza kwamba, nchini Ujerumani vijana wenye fikra za Kinazi wanajifakharisha kwa Unazi wao, na wamekuwa wakishambulia Misikiti na hata kufikia hatua ya kuwapiga na kuwauwa Waislamu wasio na hatia.

0 comments:

Post a Comment