Feb 15, 2015

JENGO LA SHULE YA AL HARAMAIN,LAPOROMOKA

Zaidi ya watu mia tano wamenusurika kifo baada ya sehemu ya jengo la ukumbi wa shule ya Al haramain kuporomoka paa lake hivi punde.
Tukio hili limetokea saa tano na dakika hamsini na sita na kushuhudiwa na Munira blog.

Mmoja wa wa fanya kazi wa jengo hilo aliidokeza munira blog kwamba jengo hilo likikua katika hali mbaya kiasi cha kushauriwa lisitumike.

Tunashukuru kuona kwamba hata hawa jamaa unao wana (UMATADA) walishalipia lakini tumewarudishia pesa yao na milango ya ukumbi tumefunga.alisema

Wakati tukio linatokea pembeni kulikua na wanachama wa umoja wa wakaazi wa Tanga waishio Dar es salaam w akifanya 
mkutano,na upande wa pili kuna waislamu zaidi ya mia mbili wakifanya dua chini ya uongozi wa sheikh Hassan chizenga.

Allah katupenda,una juwa kila juma pili sheikh chizenga anaongoza dua ndani ya ukumbi huu,hebu fikra akina mama na watoto wale wangekuwa ndani ya ukumbi 
huu,ingekua ni maafa makubwa sana,alisema Alhaj 
Abdallah Sabaya.

Katika hali isiyo ya kawaida,walinzi wa shule hiyo walimzuwia maandishi wa 
habari hizi kupiga picha.hata hivyo maandishi alifanikiwa kupiga picha kwa kutumia mbinu za kiuandishi wa habari.


Hawa ni waumini ambao wana u tamaduni wa kusoma dua kila juma pili ndani ya jengo lililoporomoka


0 comments:

Post a Comment