Feb 14, 2015

HAY ATUL ULAMAA YAMWAGA VITABU

 Baadhi ya waalimu wa Qur aan katika Madrasa mbali mbali za Jijini Dar es slaam wakipokea vitabu walivyokabidhiwa na taasisi ya HAY ATUL ULAMAA mapema leo hii,kama walivyonaswa na Kamera ya Munira Blog.

Taasisi ya HAY ATUL ULAMAA yenye makazi yake jijini Dar esalaam,leo imegawa vitabu kadhaa kwa waalimu wa Madrasa 
za Mkoa wa Dar es salaam.

Akiongea katika hafla hiyo fupi,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Suleiman Amran Kilemile amesema  ni
 Elimu pekee ndiyo inayokupeleka katika Dunia ya Maendeleo.

"Ndugu zangu Waalimu nyenzo ya kwanza ya 
maendeleo duniani ni elimu,kupitia nyenzo hii,ndiyo itakayokufikisha katika dunia ya maendeleo,kwani bila ya elimu itakua ngumu kufikia maendeleo yoyote"

Aliwaasa waalimu kuwa na juhudi ya makusudi ya kupanua elimu ili kurahisha kwa mafanikio kazi y
ao ya ufundishaji.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo Sheikh Abdallah Ndauga,aliwataka waalimu kupupia kusoma vitabu mbalimbali na kisha kuufikishia umma elimu sahihi kwa kiasio cha hitajio la Umma.

"Ndugu zangu,niwaambie kitu kimoja,hivi vitabu ni vizuri sana,lakini kuna kitabu hiki kidogo sana(Hiswnul Twiflul Muslim),bila shaka kitabu hiki,munaweza mukaona kipo chini kabisa ya mustawa wenu,lakini kisomeni na kisha wafundisheni watoto,kwa kua huu ndiyo mustawa wao,nina amini kitabu hiki kitawaimarisha sana watoto kiakhalaaq (tabia)"mwisho wa kumnukuu.

Naye Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Yasir Salim alisema "Tunamshukuru ALLAH S.W. kwani ndugu zetu wametugawia vitabu vingi sana ambapo jukumu letu lilikua ni kuvigharamia kwa pesa nyingi ili vitufikie,nasi tunavigawa bure"

Aliendelea kusema kwamba,zoezi la ugawaji wa vitabu hivi tumelianza kwa masheikh,leo tupo pamoja nanyi,aidha tutagawa na mashuleni.

aliitaja mikoa itakayo nufaika na vitabu hivyo kua ni pamoja na Tanga,Kigoma,Tabora Mwanza na Mtwara.

Jumla ya walimu wa madrasa zaidi ya khamsini wamenufaika na mgao huu ulifanyika leo katika ukumbi wa DYCC Uliopo kariakoo Jijini Dar es salaam.

HAY ATUL ULAMAA imefadhiliwa msaada 
huo wa vitabu kutoka 
taasisi ya CONVEYING ISLAMIC MESSAGE SOCIETY yenye makazi yake nchini Misri.








0 comments:

Post a Comment