Jan 7, 2015

Wachora vikatuni dhini ya uislamu wauliwa


 
Shambulio katika kituo kimoja cha magazeti nchini Ufaransam
sa wanasema kuwa wanaume waliokuwa wamejifunika nyuso wamewaua takriban watu 12 kwenye ofisi za gazeti moja la vibonzo la Charlie Hebdo.

Watu wengine watano wameripotiwa kujeruhiwa vibaya.

Gazeti hilo lililo mjini Paris limekuwa likilengwa na wanamgambo wa kiislamu siku za nyuma.

Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi wakati watu waliokuwa na silaha walipoingia katika ofisi za gazeti hilo na kuanza kufyatua risasi na kisha wakatoroka wakitumia gari.

Polisi wanafanya msako mkubwa kuwatafuta washambuliaji huku mji wa Paris ukiwa chini ya tahadhari kubwa.

Rais wa ufaransa Francois Hollande amelaani shambulizi hilo akisema kuwa nchi hiyo imepatwa na mshangao mkubwa.

Washambuliziji watatu waliokuwa wamefunika nyuso zao, walifyatuliana risasi na polisi nje ya jengo la ofisi za shirika hilo la habari kabla ya kutoroka.

Inaarifiwa washambulizi walisikika kwa sauti ya juu wakisema ''tumelipiza kisasi kw aniaba ya Mtume Muhammad.'

Rais Francois Hollande anasema hana shaka kwamba shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi
Rais Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba shambulizi hilo ni la kigaidi
Waandishi wanne wa jarida hilo la vibonzo, akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier walikuwa miongoni mwa waliouawa pamoja na maafisa wengine wawili.

Bwana Charbonnier, mwenye umri wa miaka 47, aliwahi kupokea vitisho vya kuuawa na alikuwa analindwa vikali na polisi.

Vyombo vya habari vimewataja wachoraji wengine watatu waliouawa wakiwemo, Cabu, Tignous na Wolinski. Duru zinasema shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mkutano wa kila mwezi wa uhariri wa jarida hilo.

 
 Jarida la Charlie Hebdo huangazia maswala mbali mbali kw akutumia vibonzo
 

0 comments:

Post a Comment