Baadhiya viongozi wa dini hapa nchini wamezungumzia
vurugu zilizofanywa wiki iliyopita sehemu kadhaa ya jijii Dar es Salaam na vijana
wanaosadikika kuunda kundi linalojulikana kama Panya Road.
Sheikh Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa, amesema kuwa ukosefu wa ajira ni
moja ya sababu zinazozalisha makundi ya ajabu, hivyo serikali inapaswa
kujipanga na kutengeneza mifumo ya ajira kwa vijana ili kuwaepusha
kujiingiza katika makundi tishio na hatari.
Ameongeza kuwa, vijana hao
wanavamia, kupora na kuumiza watu hovyo hovyo na kwamba ukosefu wa
ajira kwa vijana ni bomu kubwa na baya sana zaidi hata ya al Shabbab.
Naye Mchungaji Ifrahimu Mwansasu wa Kanisa la Hosana Life
Mission, amesema kwamba makundi hayo ya uhalifu yanasababishwa na malezi
mabaya ya kiimani na kitabia, kitu alichokiri kwamba hata yeye amewahi
kupitia akiwa kijana kabla ya kuokoka na kuitaka serikali ikae nao na
kujua sababu ya vijana hao kuwa hivyo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, kundi la Panya Road lilizua
tafrani kubwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwavamia, kuwapora na
kuwajeruhi watu katika maeneo mbalimbali ya mji huo, lakini Jeshi la
Polisi chini ya Kamanda Suleiman Kova lilifanikiwa kudhibiti kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment