Jan 12, 2015

Waasi wa Sudan wanawatumia watoto vitani


Waasi wa Sudan wanawatumia maelfu ya watoto kama wapiganaji vitani.

 Muhammad Musa, Mkuu wa Utendaji wa Baraza la Taifa Linaloshughulikia Masuala ya Watoto la Sudan amesema kuwa makundi ya uasi nchini humo yamewalazimisha watoto 2,100 kushirikiana nayo na kuwatumia kama wapiganaji vitani.
Musa amesema kuwa, utumiaji watoto kama wapiganaji ni kinyume na sheria za ndani za Sudan na pia za kimataifa; na kwamba wahusika wa vitendo hivyo wanapasa kuhukumiwa katika mahakama maalumu. 

Mkuu wa Utendaji wa Baraza la Taifa Linaloshughulikia Masuala ya Watoto la Sudan ameongeza kuwa, harakati za silaha za waasi zimesababisha pia watoto 8,800 kuwa wakimbizi, ambapo hivi sasa watoto hao wanaishi na familia zao makambini na katika maeneo mengine. 

Abdulrahman Hussein, Waziri wa Ulinzi wa Sudan pia mwezi Machi mwaka jana alitangaza kuwa kitendo cha waasi wa nchi hiyo cha kuwatumia watoto vitani kimesababisha jina la nchi hiyo kuingizwa katika orodha ya nchi zinazowalazimisha watoto kushiriki katika shughuli za kijeshi, na kwamba serikali ya Khartoum inafanya juhudi ili jina la Sudan liondolewe kwenye orodha hiyo.   

0 comments:

Post a Comment