Jan 12, 2015

Mshauri wa Morsi aachiwa huru kutoka jela


Morsi akiwa kizimbani Morsi akiwa kizimbani
Khaled al Qazzaz, aliyekuwa mshauri wa Rais Mohamed Morsi wa Misri ameachiwa huru baada ya kufungwa jela mjini Cairo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mshauri huyo wa zamani wa Mohamed Morsi ameachiwa huru kutokana na matatizo ya kiafya. 

Qazzaz mwenye umri wa miaka 35 na mhitimu wa shahada ya uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Toronto, Canada alikuwa mshauri wa Rais halali wa Misri Mohamed Morsi aliyepinduliwa na jeshi. 

Khaled al Qazzaz, alitiwa mbaroni pamoja na Morsi na washauri wake wengine wanane mwezi Julai mwaka juzi baada ya jeshi la Misri kumuengua madarakani Rais Morsi. 

Hata hivyo maafisa wa Misri hawakumfungulia mashtaka al Qazzaz au kutoa maelezo kuhusu sababu za kutiwa kwake mbaroni. 

Mwanasheria Mkuu wa Misri pia tarehe 29 Disemba mwaka jana aliamuru kuachiwa huru al Qazzaz, hata hivyo agizo hilo lilipuuzwa.

0 comments:

Post a Comment