Jan 7, 2015

Vijana wakikata tamaa taifa litapasuka


Ibrahim Lipumba.jpg
Serikali imeaswa kuwatumikia wananchi kwa misingi ya haki na uadilifu.

Hayo yamesemwa hivi punde na Profesa Ibrahim Lipumba alipokua akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa mtambani,magomeni mikumi jijini Dar esalaam.

Alisema uwepo wa matukio ya kiuhalifu kama panya road ni kielelezo cha vijana kukata tamaa,


Leo vijana wanapofanya biashara wanakamatwa,kiasi hawajuwi khatima ya maisha yao,wakiangalia ngazi za juu wanaona viongozi wanaiba pesa na  bila ya woga na kisha Wanagawana ndipo wanachukua maamuul magumu,alisema kwa hisia.

Aidha aliwaasa wenyeviti wapya kuwatumikia wananchi kwa haki na uadilifu,na wajiepushe na rushwa.

Ndugu zangu,ukiwa na tabia ya kupokea rushwa hauwezi kumshughulikia mtoa rushwa na haya tumeyaona hivi karibuni kwa rais wetu kushindwa kuwashughulikia mafisadi wa TegetaEscrow.

Mkutano huo ulikua ni maalumu kwa ajili ya kuwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa waliochaguliwa kwa tiketi ya chama cha wananchi Cuf

0 comments:

Post a Comment