Jan 8, 2015

Israel yazidi kuwatesa wapalestina



Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea na siasa zake za kuwatia mbaroni na kuwakandamiza Wapalestina.

Ripoti zinaeleza kuwa, jana askari wa utawala huo ghasibu ulishambulia vitongoji vya al Saila al Haditha, al Twibah na Bae'd pambizoni mwa mji wa Jenin na kuwakamata mateka vijana watatu wa Palestina.

Jeshi la Israel pia lilishambulia vitongoji kadhaa vya Wapalestina na kufanya upekuzi wa nyumba kwa nyumba na kuharibu samani ndani ya nyumba hizo.

Katika upande mwigine askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamezidisha vitendo vya kuwakamata wavuvi wa Kipalestina na baada ya makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyopita hadi sasa wamewatia mbaroni wavuvi 30 wa Palestina waliokuwa wakivua kwenye maeneo yanayoruhusiwa. 


Pia askari wa Israel wamesimamisha mashua 16 za Wapalestina na kuharibu 4. 

Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi ya Palestina Sam al A'masi amesema kuwa, kukamatwa wavuvi wa Palestina ni kukiuka makubaliano ya usitishaji vita.

0 comments:

Post a Comment